SAFARI LAGER MDHAMINI MKUU WA MICHUANO YA POOL NCHINI!!


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kwa mara nyingine udhamini wake katika mashindano ya Taifa ya mchezo wa Pool mwaka 2010. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 13 mwezi Julai 2010 katika ngazi za Mikoa.

Bia ya Safari Lager ndio mdhamini mkuu wa mashindano haya.
Akitangaza udhamini wa mashindano ya mwaka huu, Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah wa pili kutoka kulia amesema “Bia ya Safari lager imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imeweza kuleta mapinduzi ya kweli katika mchezo huu, hivyo ni dhamira ya bia ya Safari kuendelea kudhamini mashindano haya ya Taifa na mengi mengineyo ya mchezo wa pool hapa nchini. Udhamini huu unaanzia ngazi ya mikoa hadi fainali ambazo kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika mjini Arusha mwishoni mwa mwezi Septemba 2010”
Meneja huyo wa Bia ya Safari amengeza kuwa udhamini wa mwaka huu umeongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma, ikiwa ni pamoja na ongezeko la mikoa shiriki na zawadi za washindi. Akiweka wazi aina za zawadi ambazo washindi wa mwaka huu watapata katika ngazi za mikoa na Taifa Bw. Fimbo amesema.
ZAWADI NGAZI YA MKOA
ZAWADI KWA TIMU KIASI ZAWADI KWA MMOJA MMOJA KIASI (WANAUME) KIASI (WANAWAKE)
Bingwa 500,000 Bingwa 250,000 150,000
Mshindi wa pili 250,000 Mshindi wa pili 150,000 100,000
Mshindi wa tatu 150,000 Mshindi wa tatu 100,000 50,000
Mshindi wa nne 100,000 Mshindi wa nne 50,000 30,000
ZAWADI NGAZI YA FAINALI TAIFA
Bingwa 3,500,000 Bingwa 300,000 200,000

Mshindi wa pili 2,500,000 Mshindi wa pili 200,000 150,000
Mshindi wa tatu 1,500,000 Mshindi wa tatu 150,000 60,000
Mshindi wa nne 1,000,000 Mshindi wa nne 100,000 40,000

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment