Mkuu wa wilaya ya Kibaha akifungua mafunzo kwa waendesha pikipiki wilayani humo yaliyoandaliwa na kituo cha elimu Kibaha kwa kushirikiana na Kampuni ya Car & General Trading Limited ambayo ilitoa vifaa vya kujikinga na ajali kwa wa washiriki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha elimu Kibaha, Ferdinand Swai akikabidhi Kofia ya kuendeshea pikipiki na kizibao (reflectors) kwa mmoja wa waendesha pikipiki wilayani Kibaha juzi wakati wa mafunzo ya usalama kwa waendesha pikipiki yaliyokuwa yakitolewa na askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani humo juzi. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Kituo cha Elimu Kibaha kwa kushirikiana na Kampuni ya Car & General Trading Limited ambayo ilitoa vifaa vya kujikinga na ajali kwa wa washiriki.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha amewataka madereva wa pikipiki kuwa makini ili kuepuka ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha kupotea kwa maisha ya watu siku za karibuni.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waendesha pikipiki wilayani Kibaha yaliyoandaliwa na Kituo cha elimu Kibaha kwa kushirikiana na kampuni ya ya Car & General Trading Limited ya jijini Dar es Salaam, Mkuu wa wilaya hiyo Halima Kihemba alisema kuwa kwa sasa ajali zimekuwa zinaongezeka kwa kasi kiasi cha kutisha.
“Sina shaka wote mtakubaliana na mimi kuwa kwenye ajali maisha ya watu yanapotea, kukatika viungo na wengine kubakia vilema, zaidi ya hapo pikipiki ambazo ni raslimali kwa ajili ya uzalishaji kuharibika kabisa” alisema.
Mkuu huyo wa wilaya alipongeza Shirika hilo kwa kuliona athari za ajali na kuamua kushughulikia kinga zaidi kuliko tiba kwa njia ya mafunzo,” linashughulikia watu wasibakie yatima na pia wasibaki maskini kwa kupoteza mali zao”.

Aliwataka washiriki kuzingatia yote watakayofundishwa na kuwaasa “Washiriki, vifaa mlivyopewa vitumieni na kuendelea kutoa elimu kwa abiria mnaowachukua ili viweze kuleta maana iliyokusudiwa; haitakuwa na maana kuwa na kofia ukaifunga mguuni badala ya kuivaa kichwani”.
Meneja mkuu wa kampuni ya Car & General Trading Limited, Vankatesh Jayaraman alisema kampuni yake imeguswa na ajali zinazotokea nchini hususan wilayani Kibaha, hivyo kuona umuhimu wa kusaidia vifaa na uendeshwaji wa mafunzo ili kuokoa maisha ya watu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Elimu Kibaha, Kanali Ferdnand Swai alisema kuwa lengo la mafunzo haya ni kupunguza ajali na mwisho kuondokana nazo kabisa.
Takwimu zinaonyesha kuwepo kwa vifo vya watu 667 na wengine 5,525 wamejeruhiwa vibaya katika ajali za barabara zilizosababishwa na pikipiki katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi sasa. Kwa mwaka 2008, watu 282 walikufa na wengine 1,859 walijeruhiwa vibaya wakati mwaka jana idadi ya waliokufa iliongezeka na kufikia 385 huku majeruhi wakiwa 2,666.

0 comments:
Post a Comment