Mamia wauawa kwenye mkasa wa moto Bangladesh


Zaidi ya watu miamoja wamefariki katika ajali ya moto nchini Bangladesh, ulioteketeza majengo kadhaa katika eneo moja lenye watu wengi zaidi mjini Dhaka.

Zaidi ya wengine miamoja walijeruhiwa wengi wakipata majeraha mabaya zaidi.
Majengo kadhaa yaliteketezwa na moto huo uliosambaa zaidi kwa sababu ya kemikali zilizokuwa kwenye maduka ya karibu.

Moto huo ulisambaa katika majengo ya ghorofa na kuwanasa mamia ya wakaazi wa majengo hayo katika eneo moja la mji lenye idadi kubwa ya watu.

Mamlaka katika eneo hilo yamesema miili ipatayo themanini na tano imepatikana, kiini cha Moto huo ikisemekana kuwa mlipuko wa transformer.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment