CECAFA YATEUA WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MCHEZO WA TAIFA STARS NA BRAZIL JUNI 7!!


Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF limetangaza kuwa mchezo wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na timu ya taifa ya Brazil utachezeshwa na waamuzi kutoka nje ya Tanzania ambapo.

Mwamuzi wa Kati atakuwa : Mohamed Segonga - Uganda
Mwamuzi Msaidizi I: Desire Gahungu - Burundi
Mwamuzi Msaidizi II: Felicien Kabnda- Rwanda
Mwamuzi wa akiba: Charles Odan Mbaga - Tanzania
Uamuzi wa kutoa waamuzi nje ya nchi umetokana na makubaliano kati ya Tanzania na Brazil.

Waamuzi watakaochezesha mchezo huu wameteuliwa na Kamati ya Waamuzi ya CECAFA kutokana na maombi ya TFF. Wote wanatambuliwa na FIFA na wamekwishachezesha michezo mmbalimbali ya inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika CAF na Shirikisho la Soka la Dunia FIFA.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment