KOCHA MDENMARK NDIYE MRUTHI WA MARCIO MAXIMO TAIFA STARS!!

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Nchini TFF Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati alipokuwa akimtangaza kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania ambaye ni raia wa Denmark.
Amemtaja kocha huyo kuwa ni Jean Paulsen ambaye amesha chezea timu ya taifa ya Denmark na kuFundisha timu mbalimbali za taifa katika bara la Asia na Ulaya, lakini pia amesema kocha huyo ameingia mkataba wa miaka miwili kuifundisha Taifa Stars na mkataba wake anaanza mwezi Agosti.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment