BARAZIL NA TAIFA STARS ZAUNGANA KUPIGA VITA MALARIA!!

Balozi wa Brazil akiongea mbele ya wageni mbalimbali na maafisa wa mashirikisho ya mpira ya Tanzania na Brazil kwenye mkutano wa kueneza ujumbe ama kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria uliofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam leo.
Bw. Herve Verhoosel ambaye ni meneja mahusiano akimkabidhi mpira rais wa shirikisho la mpira nchini TFF Rodger Tenga kulia mpira wenye ujumbe unaohamasisha mapambano dhidi ya Malaria wakati wa mkutano wa kueneza ujumbe wa kupambana na maralia uliofanywa kwa pamoja kati ya maafisa wa timu ya taifa ya Brazil na Tanzania kwenye hoteli ya Movenpick jijinbi Dar es salaam.
Kutoka kulia ni Balozi wa Brazili Nchini Francisco Crlos Joares Luz, kiongozi wa msafara wa Timu ya taifa ya Brazil Andre Sanchez, Waziri wa Kazi Mh. Prof.Juma Kapuya na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Rodger Tenga wakiwa katika mkutano huo leo.
Waandishi wa habari wa mashirika mbalimbali ya kimataifa walioongozana na timu ya taifa ya Brazil.
Rais wa RBP kulia na Rais wa Shirikisho la Soka la Wanawake nchini Lina Muhando wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa mapambano dhidi ya Malaria.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment