Mpiganaji Athman Hamis akiongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo wakati alipokuwa kitoa shukurani zake klwa watu mbalimbali waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia katika matatizo yake mara baada ya kupata ajali.
Athman amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyoweza kumsaidia kwa hali na mali na jinsi alivyomuonyesha upendo kwa muda wote akiwa hospitali hapa nyumbani na Afrika Kusini, amesema anawashukuru pia TSN kwa kumsaidia na kutuma watu wawili kila mwezi nchini Afrika Kusini ili kumjulia hali amesema jambo hilo lilikjuwa likimfariji kwelikweli moyoni mwake.
Aakwashukuru pia mdaktari wa hospitali za Muhibili na Afrika Kusini kwa kumsaidia na kumpatia matibabu kama ilivyokuwa ikitakiwa na pia watanzania wanaoishi Afrika Kusini pamoja na wanahabari wote waliofika uwanja wa ndege kumpokea wakati alipokuwa akirejea nyumbani, katika picha kushoto ni Faith Nhlapo kutoka Afrika kusini ambaye ni Nesi anaye mhudumia kwa kila kitu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Helman Hokororo kulia akikabidhi fedha taslimu shilingi 210.000 kwa Faith Nhlapo ambaye ni msaidizi wa Athman Hamis kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini Afrika Kusinini wakati wa mkutano katika yake na wanahabari alioufanya kwa ajili ya kushukuru watu mbalimbali jinsi walivyomsaidia katika matatizo yake. katikati ni Athman Hamis mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment