Diomansy Kamara wa Fulham na Senegal atembele vivutio vya utalii Tanzania!!

Mmoja wa viongozi wa Bodi ya Utalii Mr G. Meena akimpa mchezaji Diomansy Kamara Tshirt ya Bodi ya Utalii yenye kampeni isemayo Tanzanaia The Land of Kilimanajaroa and The Seregeti akiwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Bongo Tours and Safari Mr Anold Ulomi.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal na Fulham ya Uingereza Diomansy Kamara akiongozana na mke wake wapo Tanzania kwa mwaliko wa kampuni ya Bongo Safari wakishirikianana TTB. Mchezaji huyu wa kimataifa amekuwa nchini takribani siku 9 kujionea vivutio vya Utalii vya Tanzania kwa sasa yupo Zanzibar akila maraha ufukweni kabla ya kurudi Senegal tarehe 8/June/2010. Mchezaji huyu aliwasili tarehe 31/5 na tayari ameshatembelea hifadhi ya Seregeti na Manyara, Bonde la Ngorongoro na kwa sasa yupo Zanzibar.

Wakati akiwa Arusha aliweza kutembelea maonyesho ya utalii yajulikanayo kama Karibu International Trade Fair yaliyofanyika kuanzia tareha 5-7 June 2010.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment