Bendi maarufu ya muziki wa dansi nchini FM Academia ndiyo itakayotumbuiza katika shindano la kumtafuta mrembo wa Redds Miss Ilala 2010 linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaa juni 26 jumamosi ya wiki hii.
Akizungumzia shindano hilo Mwenyekiti wa kamati ya Miss Ilala Jackson Kalikumtima amesema mambo yote yako sawa juu ya bendi hiyo na pia msanii wa ngoma za asili Wanne Star atakuwepo katika kutoa burudani katika shindano hilo litakalokua la kuvutia kutokana na mikakati iliyowekwa kuhakikisha mambo yanakuwa makubwa.
Ameongeza kuwa kwa sasa warembo wote wako safarini mkoani Tanga ambapo wanafanya ziara ya kimafunzo na tayari jana usiku walihudhuria shindano la Miss Tanga na pia wameshatembelea vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango ya Amboni na kujionea mambo mbalimbali na leo wanatarajia kuanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam.
Ameongeza kwamba kiingilio katika shindano hilo kitakuwa katika sehemu tatu ambazo vi VIP 1 shilingi laki 100.000 VIP2 shilingi elfu 50.000, na kawaida ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 10.00 kwa kila mtu, amewataka mashabiki wa urembo kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo kwani mwaka huu kiuna mambo mengi mapya ambayo watayaona na kuyafurahia.
0 comments:
Post a Comment