Rais Kikwete mgeni rasmi miaka 100 KKKT Bukoba!!

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mhashamu Elisa Buberwa akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya kanisa la Kashura mjini Bukoba kushiriki katika maadhimisho ya jubilii ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo.Katikati ni Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini Askofu Dr.Alex Malasusa (Picha na Fredy Maro).
---Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa kanisa la KKKT nchini Tanzania Askofu Dr.Alex Malasusa wakati wa maadhimisho ya jubilii ya miaka mia moja tangua kuanzishwa kwa kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa la KKKT,Kashura wilayani Bukoba mkoa wa Kagera jana mchana.

Baadhi ya waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi wakihudhuria sherehe za kuadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa kanisa hili huko Kashura Bukoba mjini jana mchana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment