AFRCAN STARS KUJIPONGEZA JUNI 27 KWENYE V IWANJA VYA LEADERS!!

Mkurugenzi wa kampuni ya ASET inayomiliki bendi ya African Stars Asha Baraka akionyesha moja ya picha za wanenguaji wa bendi hiyo wakati alipoongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo juu ya Tamasha lao wanalotarajiwa kulifanya juni 27/2010 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ili kujipongeza na mashabiki wao baada ya kuibuka na tuzo tatu za Kilimanjaro Music Award mwaka huu.

Asha Baraka amesema katika Bonanza hilo mbali ya burudani kutakuwa na michezo aina mbalimbali itakayohusisha wasanii mbalimbali wakiwemo wanamuziki, waigizaji pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu kutoka klabu mbal;imbali jijini Dar es salaam.

Ameongeza kwamba Bendi mbalimbali zimealikwa kama vile Msondo Music Band na wasanii kadhaa wa hapa nyumbani akiwemo Diamond na wengine, pia amesemakuwawako kwenye mazungum,zo na baadhiyawanamuziki wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenyea na mara baada ya mazungumzo hayo kukamilika watatangaza kuwa ni mwanamuziki gani atashirikikatika bonanza hilo

Amemaliza kwa kusema nawakaribisha mashabiki wote wa muzikihapa jijiniwajekujioneaburudanimbalimbali na kujumuika kwa pamojana wanamuziki wa African Stars katikakusherehekea tuzo hizo zaKilimanjaro Music Award ambapo kiigilio kitakuwa shilingi elfu 5.000 kwa kila mtu, katika picha kushoto ni katibu wa bendi hiyo Abu Semuhando aka Baba Diana.

African Stars ilipata tuzo tatu katika tuzo za Kilimanjaro Music Award ambazo ni Bendi bora, Albam Bora na rapa bora wa mwaka.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment