Dr. Yeronimo akizungumza mbele ya waandishi wa habari na wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa matangazo ya Redio na Televisheni kwa ajili ya kampeni ya mradi wa Champion inayoitwa "Vunja Ukimya Zungumza na Mwenzio " kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukimwi na kuweka mahusiano mema katika ya wapenzi na wanandoa ili kujikinga na maambukizi ya ukimwi, kampeni hii imezinduliwa leo kwenye Hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waandishi wa habari na wageni mbalimbali na itaendesha katika kipindi chote hiki cha Mashindano ya kombe la Dunia.
Wengine katika picha katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Engender Hearth Dr. Dunstan Bishanga na kulia ni Mradi huu unafadhiliwa na watu wa marekani kupitia shirika la USAID
Dr. Yeronimo kutoka Mradi wa Champion olio chini ya shirika la Engender Hearth akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa matangazo ya Redio na Televisheni yanayohamasisha wenza au wapenzi kuvunja ukimya na kuzungumza zaidi kuhusu mahusiano yao hasa katika kipindi hiki cha mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, Kampeni hii inaitwa "Vunja Ukimya Zungumza na Mwenzio" na kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.
Maofisa wa mradi wa Champion wakifuatilia matukio ya uizinduzi huo.
Waadisyhi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mazungumzo ya Kaimu Mkurugenzi wa Engender Hearth Dr. Dunstan Bishanga hayupo pichani.
0 comments:
Post a Comment