Zain yazindua promosheni mpya SMS- JIVUNIE!!


Zain, Kampuni ya simu za mkononi inayoheshimka kwa kutoa huduma ya mawasiliano na kusambaa maeneo mengi hapa nchini imezindua promosheni nyingine mpya kwa wateja wake ambayo itadumu kwa muda wa siku 84.

Chini ya promotion hiyo wateja wanaotumia mtandao wa Zain wataweza kujishindia fedha taslimu 500,000/- kila siku pamoja na zawadi nyingine za papo kwa hapo.

Mbali na fedha taslimu pia kutakuwa za zawadi za kila wiki ambapo wateja wa Zain watajishindia zawadi kama vile baiskeli, pikipiki aina ya Bajaj pamoja na kushinda tiketi za kushuhudia fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika huko Afrika ya Kusini.

Akitangaza uzinduzi wa promotion hiyo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Constantine Magavilla alisema kuwa Zain itakuwa ikitoa zawadi ya pesa taslimu shilingi 500,000/- kwa washindi inshirini watakaobahatika, basikeli 20 na bajaj 10, halikadhalika Toyota aina ya Corolla itatolewa kwa mshindi kila wiki.

Kwa mujibu wa Magavilla Zain vile vile itatoa tiketi 12 zilizolipiwa kila kitu za kwenda kushuhudia fainali za kombe la Dunia kwa washindi 12 watakaobahatika na zawadi kubwa katika promotion hii itakuwa ni gari aina ya RAV 4 SUV.

“Tiketi za kwenda kushuhudia fainali za Kombe la dunia zitakuwa zimelipiwa gharama zote zikiwemo za usafiri wa ndege, usafiri wa ndani wakiwa Afrika ya kusini, malazi na gharama za kuingilia uwanjani. Nnafikiri huu utakuwa ni wakati mzuri kwa wateja wetu kutembelea Afrika ya Kusini wakati wa mashindano haya makubwa ya soka ya Kombe la Dunia,” alisema Magavilla

Ili kushiriki katika promotion hii ambayo mteja atakuwa inaendeshwa katika stahili ambayo mshiriki atakuwa anajikusanyia pointi kutokana na maswali aliyoyajibu, Magavilla alisema kuwa mteja anatakiwa kujisajili kwa kutuma neno JIVUNIE kwenda namba 15656.

Baada ya hapo mteja atapata ujumbe wa kumtaarifu kuwa sasa amesajiliwa na swali la kwanza litafuatia na mwaswali mengine pia yataendelea kuulizwa ambapo mshindi atapata pointi kutokana na kujibu majibu kwa usahihi.

Pointi za upendeleo zitatolewa endapo mshiriki atakuwa amefikia kiwango cha pointi ambazo zinatakiwa, na hii inaweza kumpa nafasi ya ushindi zaidi mshiriki na kujinyakulia zawadi za kila siku na zile za mwisho wa wiki.
Magavilla alisema kuwa promosheni ni zawadi maalum kwa wateja wa Zain ambao ndiyo wameweza kuchangia mafanikio ya kampuni hiyo na kuifikisha hapa ilipo ikiwa na sifa ya moja ya makampuni ya simu za mkononi inayoheshimika kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment