WAZIRI MARMO AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA DINI LEO!

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo akiongea na viongozi wa Madhehebu ya dini kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaohudhuria mkutano wa siku mbili kujadili masuala mbalimbali yakiwemo Sheria za Uchaguzi, Uchaguzi mkuu
wa Oktoba 2010 na Mapambano dhidi ya Rushwa nchini leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Aron Msigwa - MAELEZO).
Viongozi mbalimbali wa Madhehebu ya dini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa siku mbili wa Viongozi wa Dini leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya viongozi wa dini wakichangia masuala mbalimbali leo wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam.Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na serikali kwa lengo kutoa fursa kwa viongozi wa madhehebu kujadili, kutoa maoni na ushauri kuhusu masuala mbalimbali yanayolikabili Taifa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment