Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Uturuki Mhe.. Abdullah Gul mara baada ya Spika na Ujumbe wa Wabunge wa Tanzania ambao wapo katika ziara ya nchini humo kumtembelea Ofisi kwake leo. kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Wilson Masilingi. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wanchi hiyo.kwa lengo la kuhamasisha wawekezaji katika sekata mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa nchi hizi mbili. Picha na Owen Mwadumbya wa Bunge
Ujumbe wa wabunge toka Tanzania ukiongozwa na Spika wa Bunge wa Tanzania Mhe. Samuel Sitta, ukiwa katika mkutano wa pamoja na Rais wa Uturuki Mhe.. Abdullah Gul kujadili namna ya nchi hiyo inavyoweza kusaidia maendeleo mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji toka Uturuki kuja kuwekeza nchini. Spika na Ujumbe wa Wabunge saba upo ziarani Uturuki kwa Mwaliko wa Spika wa Nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment