WATATURU WATOA BURUDANI WIKI YA UTAMADUNI SINGIDA!!

Kijana kutoka katika kabila la Wataturu akimchagua binti wa kucheza naye ngoma ya asili ya kabila hilo inayojulikana kama ngoma ya Wataturu leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya Utamaduni yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maadhimisho mkoani Singida.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Hawa ni vijana wa kike na kiume kutoka kabila la Wataturu wakicheza kwa pamoja ngoma ya asili ya kabila hilo leo mkoani Singida wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Utamaduni mwaka huu yanafanyika mkoani Singida yakiongozwa na kaulimbiu “Utamaduni ni kichocheo cha Amani.

Wacheza ngoma kutoka kabila la wataturu Wilayani Manyoni wakitoa burudani leo kwa kutumia mikono na fimbo ambazo huzipiga na kupata milio tofauti na kuifanya ngoma yao kuvutia

Hawa ni mabinti kutoka kabila la Wataturu wilayani Manyoni Mkoani Singida wakijadili jambo leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya Utamaduni inayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Maadhimisho mkoani humo.




You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Wakuu kuuliza si ujinga. Naomba kuelimishwa. 1. Je, kuna tofauti kati ya Wanyaturu na Wataturu? 2. Je, kuna jamii inaitwa watatuu? Asanteni.

Post a Comment