TBL KUBORESHA ZAIDI TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARD!!

Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro lager George Kavishe akionyesha tuzo za kisasa zitakazotolewa na kampuni hiyo kwa wanamuziki bora wa mwaka huu kwenye mkutano uliofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo kushoto ni mkurugenzi wa masoko Davidi minja
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja akionngea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo hii kwenye ofisi za kampuni hiyo

Hatimaye safari ya mchakato wa kumpata mshindi wa Tunzo za Muziki Tanzania umefikia ukingoni. ambapo.

Mchakato wa upigaji kura ulianza rasmi tarehe 1 mwezi Aprili 2010 na unaendelea hadi tarehe 13.Mei.2010. Taarifa kamili kuhusu mchakato huu unapatikana kupitia tovuti ya www.kilitimetz.com pamoja na vipeperushi na magazeti mbali mbali.


Tarehe 14 mwezi wa Mei ndio usiku wa kuwatunuku washindi katika vinyang’anyiro mbali mbali vya Tunzo za Muziki Tanzania. Usiku huu ni kwa mwaliko tu. Wana habari watapata mialiko kupitia vyombo vyao vya habari na kutakuwa na pasi maalumu kwa ajili yao ikiwa ni pamoja na eneo lao liliotengwa mahksusi kuwawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi.

Usiku huu utapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa ki Tanzania pekee. Na hao ni:

1. AY.

2. Fid Q.

3. Joh Makini.

4. Marlow.

5. African Stars – Twanga Pepeta.

6. Mwansiti.

7. Lady Jaydee.

8. Mzee Yusuph na Offside Trick

9. Wahapahapa

10. Ali Kiba


Mwaka huu Kilimanjaro Premium imeboresha zawadi pamoja na Tunzo yenyewe.

1. Zawadi za pesa taslim zitakazotolewa kwa ujumla ni TZS 15M.

2. Katika maboresho ya Tunzo zenyewe, Tunzo mbili kubwa za Hall of Fame zitakua “GOLD PLATED”.

3. Kila mteule na mshindi watapata cheti cha utambulisho wa ushiriki wake katika Tunzo za Muziki Tanzania.

Msanii Sean Kingston kutoka Marekani ndiye atapamba hafla ya Tunzo na kushiriki kwa kutoa Tunzo ya wimbo bora wa RAGGA.

Taarifa kamili na ujio wa msanii huyu zitatolewa katika mkutano na wana habari utakaofanyika tarehe 13. Mei. 2010.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment