TANZANIA YAPATA USHINDI MNONO MAONYESHO YA UTALII YA (INDABA) AFRIKA KUSINI!!

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dr. Aloyce Nzuki akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakati wa hafla iliyoandaliwa na Muungano wa Bodi za Utalii kusini mwa Afrika SADC (RETOSA) wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Utalii INDABA yaliyofanyika nchini Afrika Kusini katika jiji la Durban ambapo Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) iliibuka mshindi wa kwanza kwenye maonyesho hao yaliyoshirikisha nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Marekani Honereni TTB kwa kazi nzuri na kuiletea sifa Tanzania katika maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dr. Aloyce Nzuki akikabidhi mfuko wenye vipeperushi mbalimbali vinavyotangaza Utalii wa Tanzania vilivyochapishwa na Bodi ya Utalii Tanzania TTB kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini M/S Thokozile Xasa wakati wa maonyesho ya Kimataifa Biashara ya Utalii INDABA yaliyofanyika nchini Afrika kusini na Tanzania kuibuka kidedea katika vivutio vya utalii.
Mwakilishi wa Taasisi ya Maonyesho ya INDABA ya Afrika kusini katikati akimkabidhi cheti cha ushindi huo Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii nchini Geofrey Meena mara baada ya kutangazwa washindi katika maonysho hayo yaliyoshirikisha nchi mbalimbali, anayeshuhudia tukio hilo ni Mrs. Temu mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo kutoka Tanzania.
Moja ya cheti kinachoonyesha na kutambua ushindi wa Bodi ya Utalii ya Tanzania katika Maonyesho ya INDABA.
Banda la Tanzania linavyoonekana hii ilikuwa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Utalii INDABA yaliyofanyika nchini Afrika Kusini katika jiji la Durban.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment