Kamishna wa Jeshi la Magereza Augustino Nanyaro akiwasha Moja ya mabasi mawili yenye thamani ya shilingi milioni 320 yaliyokabidhiwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba kwa jeshi hilo kupitia Programu ya maboresho ya Sekta ya Sheria Legal Sector Reform Programme (LSRP) chini ya Wizara ya Sheria na Katiba yaliyofanyika kwenye makao makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es salaam, Mabasi hayo aina ya Isuzu yataweza kusaidia kwa kiwango kikubwa tatizo la kusafirisha Mahabusu kwenda mahakamani na kurudi mahabusu hivyo kupunguza matatizo ya uendeshaji wa kesi mbalimbali katika mahakama zetu ambazo zimekuwa zikikwama mara nyingi kwa sababu za Usafiri.
Kamishna wa Magereza Augustino Nanyaro akishuka kwenye basi baada ya kulizingdua rasmi kwenye makabidhiano ya mabasi hayo mawili kwa ajili ya kubebea mahabusu, mabasi hayo yametolewa na Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria "Legal Sector Reform Progaramme" (SLRP) kupitia Wizara ya Sheria na Katiba kwenye makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, anayeangalia ni Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Oliver Mhaiki.
0 comments:
Post a Comment