Na Evelyn Mkokoi
Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
Afisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais
Serikali ina Jukumu kubwa la kutoa Elimu na taarifa ya kutosha kwa umma wa watanzania juu ya suala zima la madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi ambayo huweza kuleta madhara makubwa zaidi katika sekta ya kilimo, wanyama pori na Mazingira kwa ujumla.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt Batilda Burian alipokuwa akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Bwana Alfonso Lenhardt, alipotembelea Ofisini kwake Mtaa wa luthuli Jijini Dar es Salaam.
Dkt Batilda ameeleza kuwa, ushirikiano uliyopo kati ya Serikali ya Marekani na Tanzania juu kupigana dhidi ya Malaria unaweza pia kutumika kama njia ya kupigana na Malaria kupitia utunzaji wa Mazingira.
“Wananchi wanaweza kupewa Elimu ya kutosha kupitia vipeperushi, vipindi vya Radio na Tv kwa lugha rahisi ya Kiswahili ili kuweza kuepukana na uharibifu wa Mazingira utokanao na ukataji miti na kilimo holela, Alisema.”
Akitolea mfano, Uharibifu wa Mazingira kwa upande wa Ziwa Victoria, Balozi wa Marekani Nchini, Bwana Alfonso E. Lenhardt amesema kuwa madhara mengi yanasababishwa na nchi jirani kwani Tanzania haitegemei zaidi ziwa Victoria pekee kwa uvuvi kutokana na utajiri wa maziwa mengi yaliyopo nchini, pamoja na Bahari ya Hindi.
Akitolea mfano wa Nchi zilizoendelea ambapo matumizi ya nishati ya jua yapo juu zaidi, Balozi Lenhardt, ameshauri kuwa,ni wakati muafaka sasa kwa Tanzania kufikiria zaidi matumizi ya nishati mbadala ili kuweza kunusuru Mazingira.
0 comments:
Post a Comment