Chuo Kikuu cha Egerton cha nchini Kenya juzi kilitinga hatua ya nusu fainali ya mashindano yanayoendelea ya Zain Africa Challenge, chemsha bongo ya mtoano ya kimataifa ya Vyuo kwa vikuu baada ya kuwashinda wapinzani wao Chuo Kikuu cha Maiduguri cha Nigeria.
Egerton waliibuka washindi baada ya kupata jumla ya pointi 710 dhidi ya wapinzani wao Maiduguri waliopata pointi 650.
Kufuatia ushindi huo, Chuo Kikuu cha Egerton kinaungana na wenzao Chuo Kikuu cha Africa Nazarene cha Kenya na Chuo kiku cha Makerere cha Uganda ambao tayari wamekwisha fuzu hatua ya nusu fainali.
Kufuatia ushindi huo, Chuo Kikuu cha Egerton kinaungana na wenzao Chuo Kikuu cha Africa Nazarene cha Kenya na Chuo kiku cha Makerere cha Uganda ambao tayari wamekwisha fuzu hatua ya nusu fainali.
Mchuano wa mwisho wa robo fainali utafanyika jumapili ijayo kati ya Chuo Kikuu cha Chuo Kikuu cha Jommo Kenyata cha Kenya na Chuo Kikuu cha Copperbelt cha Zambia. Baada ya hapo mashindano hayo yatatinga hatua ya nusu fainali.
Vyuo Vikuu vinane kati ya 16 vilivyofuzu kuingiakatika fainali za ZAC ndivyo vinavyowania nafasi ya kuingianusu fainali itakayoshirikisha Vyuo Vikuu vinne kabla yafainali ambayo itashirikisha Vyuo Vikuu viwili ambavyovitakuwa vinawania ubingwa pamoja wa kitita cha dola za marekani 50,000.
Meneja uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta alisema jana jijini Dar es Salaam kuwaWatazamaji wa Zain Afrika Challenge bado wanafursa ya kushiriki katika mchezo wa Zain kupitia SMS.
“Wateja wa mitandao yote nchini wanaruhusiwa kishiriki,Wanachotakiwa kufanya ni kujibu maswali yanayoulizwa wakati na mtoano na kujishindia zawadi ya simu mpya za mkononi aina ya Nokia N97 yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane,” alisema Mutta.
Alisema kuwa ili kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda 15315.
Alisema kuwa ili kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda 15315.
Kwa mujibu wa Mutta, zawadi hizi zitaendelea kutolewa kila wiki ambapo Zain itachagua washindi watatu wa simu hizo kila wiki.
Jumla ya Vyuo Vikuu 100 kutoka nchi nane barani Africa ambazo ni Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia vilichuana katika mtoano wa kitaifa kabla ya kuingia raundi ya kwanza ya fainali ya mtoano wa ZAC nchini Uganda.
Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain zinazolenga kuboresha sekta ya elimu na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhawa kwa wateja wa Zain.
0 comments:
Post a Comment