Kampuni ya Kapito Leterz Entertainment imetangaza zawadi kwa washindi washindano la RBP Miss Dar Inter College linalotarajiwa kufanyika tarehe 27 Mei kwenye ukumbi wa Billicanas jijini Dar es salaam.
Akitangaza zawadi hizo mratibu wa RBP Miss Dar Inter College Silas Michael amesema mshindi wa kwanza ataondoka na shilingi milini 1,500,000, mshindi wa pili atapata shilingi Milioni 1,000,000, mshindi wa tatu atapata shilingi laki 500,000, mshindi wa nne atapata shilingi laki 400,000, mshindi wa tano atapata shilingi laki 300,000 na washiriki wengine watapata shilingi laki 200,000 kila mooja kama kifuta jasho.
amesema wametoa zawadi hiyo nono ya fedha ili kuwasaidia warembo hao kwani wako vyuoni wanasoma na hivyo zawadi hizo zitawasaidia katika kulipa karo na matumizi mengine ya shuleni.
Ameongeza kuwa wanamuziki Elias Barnaba na Amini Mwinyimkuu kutoka kundi la THT watatumbuiza katika shindano hilo linalovuta hisia za wapenzi wa urembo jijini Dar es salaam ambapo warembo 15 wanatarajiwa kuchuana vikali jukwaani.
Wadhamini wa shindano hilo ni RBP Oil & Industrial Technology T Limited, Billicanas, Tanzania Daima, Redds Original,Vodacom Tanzania, Shear Illusion, Ndege Insurance, Michuzi, Janejohn5,Mtaa kwa Mtaa, Fullshangwe.blogspot, Dotnata Decorations, Clouds Fm na Condy Bureau de Change.
0 comments:
Post a Comment