RAHMA GEGE AIBUKA VODACOM MISS IRINGA 2010!!

Vodacom Miss Iringa Rahma Gege (kati) akiwa na Grace Simon (shoto) na Maria Kagali baada ya kutangazwa washindi wa Vodacom Miss Iringa 2010.
Rahma Gege aliibuka Vodacom Miss Iringa 2010 kwenye shindano lililofanyika St. Dominic karibu na Ruaha University College Iringa Mjini siku ya Ijumaa 21/05/2010 akifuatiwa na Grace Simon aliyekuwa mshindi wa pili na Mary Kagali kama mshindi wa tatu.
Nne bora wakiwa kwenye picha ya pamoja

Shindano hilo lilihudhuriwa na Mheshimiwa Amani Mwamwindi - Meya wa Manispaa ya Iringa - ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kusini Bw. Jackson Kiswaga na wafanyakazi mbalimbali wa Vodacom Kanda ya Kusini na Makao Makuu DSM pia walikuwepo katika shindano hilo.


Kushoto Wadhamini wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Vodacom Miss Iringa.
Kulia Wafanyakazi wa Voda Domician Mkama, Elihuruma Ngowi na Alex Mlay walikuwepo kushuhudia show hiyo kali sana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment