RAIS WA RBP OIL INDUSTRIAL TECHNOLOGY LTD AWAPONGEZA (TWIGA STARS) KWA USHINDI DHIDI YA ERITREA!!

Meneja wa Huduma wa kampuni ya RBP Oil& Industrial Technology Limited Ibrahim Khatrush akizungumza na wanahabari katika mgahawa wa Hadees leo kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Fredrick Mwakalebela.

Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology Tanzania Limited inaipongeza timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars kwa ushindi wa magoli nane kwa moja ilioupata dhidi ya timu ya taifa ya Eritrea katika mchezo wake wa awali wa kombe la mataifa ya Afrika jana mei 23 kwenye uwanja wa Uhuru.
RBP ikiwa mdhamini mkuu wa timu hiyo ya taifa ya wanawake inaamini kwamba ushindi huo umetokana na juhudi za dhati za mwalimu pamoja na wachezaji wa timu hiyoTwiga Stars ambao waliahidi kwamba watafanya vyema katika mchezo huo.
Salamu hizi zinatoka kwa Rais wa kampuni ya RBP Madame Rahma Al Kharoos ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani na ameahidi kuwapa zawadi kubwa wachezaji wote wa Twiga Stars pamoja na viongozi wao kwa juhudi kubwa walizozifanya na kupata ushindi huo mnono.
Madame Rahma akiwa nchini Marekani anaendelea na maandalizi ya kambi ya timu hiyo na kutafuta mechi za majaribio kwa timu hiyo ya Twiga Stars wakati itakapokuwa nchini humo.
Madame Rahma anasema RBP kama wadhamini wakuu na ikiwa walitoa shilingi milioni kumi za maadalizi ya mchezo dhidi ya Eritrea anaahidi kwamba wataendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo katika harakati zake za kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika Septemba mwaka huu chini Afrika Kusini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment