Rais Kikwete awaapisha wajumbe wa Tume ya ya maadili ya Uongozi na kukutana na Mkuu wa utawala wa UNDP Helen Clark Ikulu jijini Dar es salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Jaji Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na wajumbe wa tume hiyo katika sherehe zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wajumbe wa tume hiyo ambao pia waliapishwa ni pamoja na Jaji Hamis Msumi na Ndugu Gaudios Tibakweitira.Pichani Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kupokea miongozo ya kazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Tume ya Maadili ya uongozi muda mfupi baada ya kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto ni Jaji Hamis Amir Msumi,Ndugu Gaudios Tibakweitira na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na mkuu wa utawala wa UNDP Bibi Heken Clark ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment