RAIS KIKWETE AMEMTEUA BWANA DEOS MNDEME KUWA POSTA MASTA MKUU WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO.
Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Deos Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania kuanzia mwezi Aprili, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt Florens Turuka imesema kuwa, Bwana Mndeme alikuwa kaimu Posta Masta mkuu kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Bwana Mndeme alikuwa ni mfanyakazi wa shirika hilo kwa muda wa takribani miaka thelathini lililoanzishwa kufuatia kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment