Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo akitoa ufafanuzi leo jijini Dar es salaam kwa waandishi wa habari juu ya uchangia wa bajeti unaofanywa na wafadhili. Wengine ni Afisa wa fedha za Nje Matembele ( kulia kwa Waziri) ,Msemaji wa Wizara wa Wizara hiyo Bibi Ingiahedi C. Mduma(wa pili kulia kwa Waziri) na Kamishina wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya (wa tatu kulia kwa Waziri)
Katika maelezo yake waziri amesema wafadhli hao wamekuwa wakichangia kiasi cha dola za kimarekani milioni 754 mwaka 2009 - 2010 akasema kwa mwaka wa fedha wa 2010-2011 kiwango cha uchangiaji wao kitapungua mpaka dola za kimarekani milioni 534 ikiwa ni pungufu ya dola milioni 220 katika bajeti ya serikali.
Amesema kupungua kwa msaada huo kumetokana na kwamba wafadhili hao walitukopesha fedha wakati wa mtikisiko wa kiuchumi duniani ili deni hilo likatwe katika mgao wa fedha ambazo watatupa katika kipindi cha bajeti cha 2010-2011 ambapo amefafanua kwamba bajeti yote kwa mwaka ni asilimia 40 wakati uchangiaji wa wahisani ni asilimia 12 tu.
amesema hayo serikali iliyajua toka mwaka jana mwezi wa Novemba hivyo ilijiweka sawa ili kukabiliana nalo na tayari serikali imejizatiti kwani imeshakubaiana na Benki ya Stambic ya hapa Tanzania, Afrika Kusini na Uingereza na matawi hayo yote kwa ujumla yamekubali kuikopesha Serikali kiasi hicho cha dolla milioni 220 kwa ajili ya kufidia katika pengo la bajeti ijayo.
Moja ya matatizo yaliyoainishwa na wahisani hao ambayo serikali imetakiwa kuyafanyia kazi ni uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji nchini jambo ambalo limekuwa likikwamisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza nchini ikiwemo mambo ya usajiri wa makampuni kuchukua muda mrefu, ucheleweshwaji wa kutoa mizigo bandarini na upatikanaji wa ardhi kwa haraka kwa wawekezaji hao.
0 comments:
Post a Comment