Pichani juu ni Mhe. Waziri wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja, akitoa hotuba maalunu katika kongamano hilo asubuhi ya leo Picha na habari Veronica Simba wa nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Mganga Ngeleja, leo ametoa hotuba iliyojikita kwenye masuala ya Biofueli na uendelevu wake kwa mtazamo wa Tanzania, hapa Sevilla nchini Hispania akimwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Kongamano la Kimataifa la Biofueli, 2010.
Kongamano hilo litakalodumu kwa siku mbili, limewaleta pamoja viongozi wa sekta za viwanda, wawakilishi wa serikali na asasi zisizokuwa za kiserikali, wakichambua na kujadili masuala ya Biofueli ulimwenguni ili kurejesha matumaini kuhusu umuhimu wa biofueli na kubainisha mikakati mahususi itakayofanikisha biashara yake na uendelevu wa muda mrefu wa sekta hii.
Kongamano la Kimataifa la Biofueli 2010, ni la tisa katika mfululizo wa makongamano ya aina hii yanayoandaliwa kila mwaka na taasisi za F.O. Licht na Focus Abengoa Foundation.

0 comments:
Post a Comment