Mosses Malapela a.k.a Shumba Ratshega, kiongozi wa kundi la Makhirikhiri: Kutoka pande za Botswana ambaye ni staa wa muziki wa asili, amewaongoza wakali kadhaa wa muziki huo kutoka kwenye kundi lake wakati walipowasili jioni hii kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere kwa ajili ya maonyesho kadhaa katika mikoa kadhaa na jijini Dar es salaam katika ziara ambayo inaratibiwa na kituo cha radio cha Times cha jijini Dar, kulia ni mmoja wa waratibu wa ziara ya msanii huyo kutoa Kituo cha redio cha Times Fm Scolastica Mazula, lakini wadau wenzangu nasisitiza kwamba kuchukua picha haikatazwi lakini ni muhimu kutambua mchango wa blog au chanzo cha habari ambayo imetoa hizo habari ama picha na kukipa crediti ni muhimu sana hilo.
Hapa mwanamuziki huo mkali wa muziki wa asili akiongoza na na mwenyeji Scolastica Mazula kutoka Times Fm aliyempokea mara baada ya kuwasili jijini Dar.
Mosses Malapela kushoto akicheza na Wanne Star mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere na kuvishwa mgolole na wanne star kama shujaa wa muziki wa asili.
Msanii wa ngoma za asili Wanne Star akinyanyua mkono huku akiwa ameshikana mkono na Mosses Malapela kiongozi na Staa wa kundi la Makhirikhiri Kutoka pande za Botswana ambaye ni staa wa muziki wa asili, Moses Malapela a.k.a Shumba Ratshega, amewaongoza wakali kadhaa wa muziki huo na kutua jijini Dar leo.
0 comments:
Post a Comment