Bilioni 11 kusaidia upatikanaji wa umeme Afrika!!

Makamu Rais anayeshughulikia Miundombinu na Sekta binafsi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Bobby Pittman(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Abidjan juu ya miradi 26 ya umeme yenye thamani ya dola bilioni 11 inayotarajiwa kuendelezwa katika nchi mbalimbali barani Afrika. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Jinsia, Mabadiliko ya Tabia Nchi na Maendeleo Endelevu wa ADB Dkt Antony Yong(kulia) na Mkurugenzi wa Nishati , Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi wa ADB Bibi Hela Cheikhrouhou(kushoto)
Na Tiganya Vincent, Abidjan

Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) inatarajia kutumia dola bilioni 11 kwa ajili ya kuendeleza miradi 26 ya umeme katika nchi mbalimbali barani Afrika

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Abidjan na Makamu Rais wa ADB anayeshughulikia Miundombinu na Sekta Binafsi Bobby Pittman wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya benki hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Alisema kuwa fedha hizo zinatarajiwa kuendeleza miradi uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu ya upepe na nguvu ya maji.

Bw. Pittman alisema kuwa lengo la ni kutaka kupunguza tatizo la nishati ya umeme katika maeneo mbalimbali ya Afrika na hivyo kusaidia na uharibifu wa mazingira unaotokana na utafutaji wa nishati kwa ajili ya matumizi ya kila siku.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Jinsia, Mabadiliko ya Tabia Nchi na Maendeleo Endelevu wa ADB Dkt. Antony Yong alisema kuwa Benki hiyo inazo fedha za kusaidia harakati za uhifadhi wa mazingira na hivyo ni jukumu la kila nchi kuomba ilionyesha mahitaji halisi na mikakati itakavyotumia katika uhifadhi wa mazingira.

Aidha aliongeza kuwa Benki hiyo inatilia mkazo wa uhifadhi wa bonde la Kongo kwa kuwa ni chanzo kikubwa cha upatikanaji wa maji kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya umeme wa maji ya kupunguza gesi ya ukaa.

Mkutano 45 wa ADB ulioanza jumatatu utafunguliwa leo(Alhamis) na Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment