Mwanamuziki Adolf Domingize wa Wenge Musica Tonyatonya akipungia mkono mashabiki wake wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jioni hii kwa ajili ya utambulisho rasmi wa bendi ya Extar Bongo utakaofanyika kwenye ukumbi wa Msasani Club siku ya ijumaa mei 28 huku kiingilio kikiwa shilingi elfu kumi kawaida na elfu kumi na tano viti maalum kulia ni kiongozi wa bendi ya Extra Bongo Ali Choki aliyempokea ila nawaomba wadau wenzangu wa blog na magazeti tamueni mchango wa wenzenu hivyo mnapochukua picha jaribuni kutoa credit kwa yule aliyetafuta habari tunakumbushana ni muhimu sana.
Adolf akisalimiana na msanii wa ngoma za asili kutoka Tanzania Wanne Star kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere katikati ni promota wa mwanamuziki huyo Julius Nsana.
0 comments:
Post a Comment