MIUNDO MBINU YA AFRIKA KUTUMIA DOLA BILIONI 6!!


Benki ya Maendeleo ya Afrika iliidhinisha kiasi cha dola za kimarekani bilioni 6 kwa ajili ya miundo mbinu ya kisasa kwa nchi wanachama. Hayo yalisemwa na Bw. Thierry de Longuemar ambaye ni Makamu wa Rais wa Mabenki ambaye pia ni Mkuu kwa upande wa mambo ya fedha,katika mada yake iliyoelezea taarifa za fedha kwa mwaka 2009 mapema jana katika mkutano wa mwaka wa mabenki.


Katika mwaka huo wa 2009 miradi ya miundo mbinu iliyopata pesa ni pamoja na miradi ya viwanja vya ndege vya Morocco na Tunisia, miradi ya barabara ya Burkina Faso, Cameroon, Chad, Ghana, Guinea, Mali, Sierra Leone, Malawi, Rwanda, Senegal na Uganda.
Mingine ni ile inayounganisha barabara za nchi ya Cameroon-Nigeria, Cameroon-Gabon, Kenya-Ethiopia and Mozambique-Malawi-Zambia.

Aidha Bw. Longuemar, alieleza kuwa mradi mwingine uliopitishwa ni mradi wa umeme wa Botswana, Kenya, Lesotho, Nigeria, South Africa na Tunisia.
Pia mradi wa sekta ya maji wa Tunisia, Morocco and Egypt ulipitishwa na benki mwaka 2009.
Sekta binafsi kwa mwaka 2009 zilipatiwa kiasi cha dola za kimarekani billioni 1.8 (UA1.16 ), kutoka kiasi cha dola za kimarekani billion 1.4 (UA901) mwaka 2008.

Miradi mingine iliyosaidiwa ni kama ile ya kusaidia biashara iliyotolewa huko Ghana ambapo dola za kimarekani million 35 zilitolewa katika kusaidia soko la nje la uvunaji cocoa kwa mwaka 2009; dola za kimarekani million 5 zilitolewa kama mkopo kwa benki ya maendeleo na uwekezaji huko Liberia na dola za kimarekani millioni 55 kwa ajili ya mambo ya baharini na mambo ya viunganishi vya mitandao.

Kwa upande wa kikanda , Benki ilipitisha kiasi cha dola za kimarekani milioni685 (UA453.2) ambazo zilikuwa kwa ajili ya maendeleo ya miundo mbinu, kwa ajili ya kuvijengea uwezo vyuo, kwa ajili ya kudumisha umoja wa Afrika , kuimarisha uchumi wa Afrika,kwa ajili kuimarisha kamisheni za uchumi Afrika , kupitia uandaaji wa bajeti pamoja na manunuzi ya umma.
Aidha benki ilipitisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 551(UA 364.8) mwaka 2009 kusaidia nchi za Guinea-Bissau, Togo, Cote d’Ivoire, Liberia, Sierra Leone, Comoros na Central Africa Republic ambazo zilikuwa na matatizo ya kifedha.

Akielezea utendaji na uwezo wa benki katika kusaidia hapo baadae De Longuemar alisema kuwa benki inauwezo wakukidhi mahitaji alimradi tu kuwe na mtaji wa kutosha ambao utawezezesha kusaidia kila nchi yenye kupata tatizo.

Alimalizia kwa kusema kuwa katika miaka hii miwili, Dola za kimarekani billioni 1 zilizowekwa kama rehani na Benki ya Afrika zimekuwa na mafanikio makubwa wakati Benki ya maendeleo ya Afrika ikiendelea kuwa na soko imara la dola. Alieleza kuwa fedha hizo zimekuwa kivutio cha kusababisha mahitaji ya kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1.44 na asilimia 75 ya fedha hizo ilitoka benki kuu”. alieleza mtaalamu huyo katika taarifa hiyo ya mahesabu ya benki.
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu-Wizara ya Fedha na Uchumi
Abidjan
26.05.2010

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment