Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akikabidhi Hundi yenye Thamani ya shilingi Mil. 12 kwa Mratibu wa Shindano la Miss Dar Inter College,Silas Michael huku warembo washiriki wakishuhudiaa.(picha na Othman Michuzi)
Warembo wa Miss Dar Inter College wakiwa katika picha ya pamoja na Mdhamini wao,Mama Rahma Al Kharoos leo katika viwanja vya Hotel ya Movenpic.(picha na Othman Michuzi)

KAMPUNI ya RBP & INDUSTRIAL TECHNOLOGY TANZANIA LIMITED ya jijini Dar es Salaam leo imetangaza kudhamini shindano la Miss Dar Inter College na imeweza kutoa kiasi cha shilingi milioni 12 kwa ajili ya zawadi za warembo wanaowania taji hilo litakalofanyika May 27 kwenye klabu ya kimataifa ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo ni kutoka vyuo vya mbali mbali vya elimu ya juu vya jijini Dar vikiwemo CBE, IFM, DSJ, TSJ, ISW
Akiongea na Waandishi wa habari waliofika katika mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Movenpic,Rais wa Kampuni hiyo ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY TANZANIA LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos alisema.”Kampuni yangu ya RBP ni ya kizalendo na imeona vyema kuwasaidia warembo hawa ambao ni wasomi na pia ni taifa la kesho na ambao wataweza kuleta maendeleo katika nchi yetu kupitia fani hiyo ya urembo”.

Aliendelea kusema “Ninawapa msaada huu Warembo hawa kama wanangu na hivyo kama Mama ninaejali familia na watoto kwa ujumla nimeona leo niweze kuwasaidia katika kufanikisha kupatikana kwa zawadi zitakazoweza kuwanufahisha maishani mwao.”
Msaada huo ni mwendelezo tu wa kusaidia na kuinua vipaji vya wasichana hapa nchini ambapo juzi tu Mdhamini huyo aliweza kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa timu ya taifa ya wanawake ‘TWIGA STARS’ ambayo inajiandaa na kucheza michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake.
Twiga itacheza na timu ya taifa ya Elitrea May 23 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo unaotazamiwa kuwa na upinzani mkali
Kwakumalizia Mama Al Kharoos aliwahusia warembo hao kwa kuwataka waepukane na vishawishi na mambo yasiyofaa katika Jamii pia wawe na tabia njema waapo majumbani mwao. Kwani kujiheshimu kwao ndiko kutakapo wapatia heshima katika sehemu yoyote ile watakayokuwepo.
RAHMA AL KHAROOSI
President – RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY

0 comments:
Post a Comment