Mwanadada Lady Jay Dee akiimba wakati wa onesho la bendi yake lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye klabu ya Arabela Masaki jijini Dar es salaam, ukumbi huo ulifurika mashabiki lukuki huku wakijimwaga kule na huku wakati zikipigwa nyimbo mbalimbali na mwanamuziki huyo nyota nchini.
Akina dada mbalimbali wakadatishwa na mwanadada Lady Jay Dee wakanyanyuka na kulisakata dansi kisawasawa ilimradi kila mtu kujipa burudani na shangwe.
Vijana wa Machozi Band wakilishambulia jukwaa kwenye klabu ya Arabela jana usiku ambapo kulifurika mashabiki lukuki kama vile ndiyo wikiendi inaanza.
0 comments:
Post a Comment