IGP Said Mwema akihojiwa na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Wizara ya Mambo ya Ndani mara baada ya kusaini mkataba huo jana.
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi DAR ES SALAA
,
Serikali ya Korea Kaskazini, imeahidi kulisaidia Jashi la Polisi hapa nchini katika Nyanja mbalimbli zikiwemo za mafunzo ya upelelezi dhidi ya makosa ya kigaidi na yale yatokanayo na wizi kupitia mifumo ya mitandao ya kompyuta.
Ahadi hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Balozi wa Korea hapa nchini Bw. Jae Young Kim, wakati wa hafla fupi ya kulitiliana saini makubaliano hayo iliyofanyika Makao makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam.
Bw. Kim ambaye ni Afisa wa Ubalozi huo wa Korea kaskazini hapa nchini, amesema kuwa, kutokana na mabadiliko ya teknolojia na jitihada zinazoonyeshwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania katika kukabiliana na makosa mbalimbali Serikali ya Korea kupitia Kampuni ya Misaada kwa nchi za Kiafrika ya Koica, itasaidia kuwapatia elimu na ujuzi mbalimbali makachero wa Jeshi la Polisi ili kuwawezesha kukabiliana na mageuzi na mbinu mpya zinazotumiwa na wahalifu wa Kimataifa.
Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Koica, Bw. Sungsoo Oh, Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa kwa muda mrefu Jeshi lake limekuwa katika mchakato wa maboresho na kwamba misaada hiyo ya kimafunzo inakwenda sambamba na maboresho ya Jeshi hilo yanayoendelea hivi sasa.
Aidha IGP Mwema amewaagiza Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa na Wilaya, kuandaa mahitaji ya kimafunzo na kuyawasilisha kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili taratibu za mchakato wa mafunzo hayo zianze mara moja.
0 comments:
Post a Comment