Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka kulia akimkabidhi bahasha ya pesa Taslimu shilingi milioni 1.7 Kiongozi wa bendi ya African Stars Lwiza Mbutu ambazo walipewa wakati waliposhinda na kuchukua tuzo tatu kwa mpigo kwenye Kilimanjaro Music award hivi karibuni zilizofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam hivi karibuni katika sherehe ya kuwapongeza wanamuziki wa bendi hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Mzalendo Pub na kuhudhuriwa na watu maarufu mbalimbali wakiwemo waigizaji, wanamuziki, Wakurugezni wa makampuni na watangazaji na mashabiki wa bendi hiyo.
Mambo ya Twanga hayo mdau kwa sasa wako juu sana .
Vimwana wa Twanga pepeta wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mwanamuziki wamuziki wa kizazi kipya Diamond ambaye pia alishinda tuzo tatu kwa mpigo kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award akicheza na mmoja wa mashabiki waliokuwepo katika sherehe ya kuwapongeza wanamuziki wa African Stars jana usiku pale Mzalendo Pub Makumbusho.
New Zamzibar Stars Molden Taarab wakifanya vitu vyao jukwaani katika sherehe hiyo.
Hapa ni kama Steve Nerere anabembeleza kitu vile hebu mcheki mdau.
Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Kanumba, Steve Nyerere, Sam Machozi wa Machozi Band, Sylivia Miss Ilala 2009 na jaquiline wakila pozi mbele ya Camera ya kamanda wa FULLSHANGWE.
Mdau Abdalla Mrisho wa Grobalpublishers kushoto na Mdau Khadija Khalili kutoka Tanzania Daima wakipata menyu.
Rafiki yake mwanamuziki Furgason ambaye ni rapa wa bendi ya Twanga Angela Bushoke akimsalimia mamaa Dotnata huku Furgason aliyesimama kushoto akiangalia.
0 comments:
Post a Comment