Mshauri wa ufundi kuhusu masuala ya HIV na UKIMWI mahali pa kazi katika sekta za umma (Technical Advisor supporting Public sector workplace on HIV and AIDS) Dr. Fidelis Owenya akimkabidhi na vipeperushi mbalimbali vinavyotoa elimu juu ya kujikinga na kupambana na UKIMWI jana mjini Bagamoyo kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari , Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko. Vitabu hivyo vilitolewa wakati wa mafunzo ya siku moja kwa viongozi waandamizi na watumishi wa Wizara hiyo ya sehemu ya kudhibiti maumbikizi mapya kwa wafanyakazi wake na kuwasaidia watakaobainika kuwa na maambukizi
Na Tiganya Vincent-Bagamoyo
Wizara ya Habari , Utamaduni na Michezo imeandaa utaratibu wa kuwasaidia wafanyakazi wake ambao watapima kwa hairi na kuueleza uongozi kuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha ili waweze kuishi muda mrefu na kuendelea kutoa mchango wao katika Wizara hiyo na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Bagamoyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Professa Hermas Mwansoko wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya siku moja ya viongozi waandamizi na wanfanyakazi wa Wizara hiyo.
Alisema kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni na michezo imetenga bajeti kwa ajili ya kuwahudumia watumishi wake ambao watakuwa tayari kujitokeza kupima afya zao na kama watagundulika na maambukizi waweze kupata huduma zinazostahili mapema.
Professa Mwansoko alisema kuwa wameaanda utaratibu wa kutoa dawa na chakula kwa ajili ya wafanyakazi wao ambao watagundulika wana maambukizi.
Aliongeza kuwa huduma nyingine ni pamoja na kumpunguzia kazi ili ziwiane na hali ya afya yake.
"Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa tunawakinga watumishi wetu wasipate maambukizi mapya kwa wale ambao bado hawajapata halikadhalika kuwahudumia wale waliopata maabukizi kwa kuwtafutia dawa ,kuwapa chakula kwa ajili ya lishe, alisistiza Kaimu Katibu mkuu huyo.
Alisema kuwa sanjari ya kinga wanaendesha wafunzo kwa watumishi wote kwa lengo la kuwapa mbinu za kujikinga, kubadili tabia na kuwafanya wasije wakawanyanyapaa wale wote wataojitokeza kujitanga kuwa wanaishi na VVU.
0 comments:
Post a Comment