NGORONGORO HEROES YAWALAZIMISHA WAMALAWI SULUHU YA 2-2!


Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ngorongoro Hiroes iliyokuwa na kibarua kigumu dhidi ya timu ya taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Malawi leo imetegua kitendawili baada ya kulazimisha sare ya magoli mawili kwa mawili dhidi ya timu hiyo ya wamalawi katika mchezo uliochezwa nchini humo leo.

Kwa matokeo hayo timy ya Ngorongoro Heroes inajiweka katika nadfasi nzuri ya kusonga mbele endapo itashinda katika mchezo wake wa marudiano utakaofanyika wiki mbili zijazo jijini Dar es salaam.

Kwa vyovyote vile matokeo haya yanaiweka Ngorongoro Heroes katika rekodi nzuri kwani katika michezo yake mingi iliyocheza imefanya vizuri kama vile ilipokwenda Brazil, Afrika Kusini katika mashindano ya Copa Cocacola, Sudan na hata ilipocheza na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars chini ya Umri wa miaka 20 ikashinda magoli manne kwa matatu kitu ambacho kinaifanya iwe na rekodi inayoleta matumaini katika siku za usoni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment