Wataliano wawili mtu na mkewe waliokuwa wakishikiliwa mateka nchini Mali na kundi la al-Qaeda katika nchi za Kiislamu za Maghreb wameachiliwa huru.
Maafisa nchini Mali wamesema Sergio Cicala na Philomene Kaboure walichukuliwa na wanajeshi waliokuwa wakipiga doria mkoa wa Gao mashariki mwa nchi hiyo.
Maafisa nchini Mali wamesema Sergio Cicala na Philomene Kaboure walichukuliwa na wanajeshi waliokuwa wakipiga doria mkoa wa Gao mashariki mwa nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia amesema, raia hao wa Italia kwa sasa wapo "mikononi mwa serikali ya Mali" na wamepelekwa sehemu iliyo "salama".
Bw Cicala na Bis Kaboure ambaye pia ana uraia wa Burkina Faso walikamatwa mwezi wa Disemba nchi ya jirani ya Mauritania.
Wanandoa hao walikuwa ndani ya gari lao kupitia mji wa mashariki wa Kobenni tarehe 18 mwezi wa Disemba wakielekea Burkina Faso kumuangalia mtoto wa Bi Kaboure mwenye umri wa miaka 12 ndipo walipotekwa na watu waliokuwa na silaha
0 comments:
Post a Comment