TIMU YA WANAWAKE SIMBA HII HAPA!!

Klabu ya SIMBA imetambulisha timu yake ya soka kwa wanawake wenye miaka 12 hadi 17 ambapo imewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu wanapokuwa katika michezo mbali mbali.


Akizungumza kwenye utambulisho wa timu hiyo katika uwanja wa KARUME, Katibu mkuu wa SIMBA MWINA KADUGUDA amesema kuwa mchezaji akiwa na nidhamu anaweza kuenedelea katika soka kama timu ya SIMBA ilivyo.

Timu hiyo inajiandaa kushiriki katika mashindano ya wilaya ya ILALA ya soka la wanawake inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kwa upande wake mwanzilishi wa timu hiyo STEPHANIA KABUMBA na kocha wa wachezaji hao ANTONY MAKUNJA wamesema wachezaji hao wanajitahidi kufanya vyema kwenye mazoezi na kudai kuwa watahakikisha timu hiyo inaendelea zaidi ili kupata wachezaji wazuri watakakwenda kwenye timu ya TAIFA ya wanawake habari na picha kwa hisani ya www.janejohn5.blogspot.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment