Maelfu ya watu wanatarajiwa kukusanyika katika mji wa Kracow nchini Poland hii leo kwa mazishi ya kitaifa ya Rais Lech Kaczynski, aliyefariki dunia katika ajali ya ndege magharibi mwa Urusi.
Baada ya kufanyika kwa misa iliyohudhuriwa na watu wengi kwa wahanga waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo, rais atazikwa pamoja na mkewe katika chumba katika Kanisa la Wawel, ambalo lilitumika kuwazika wafalme na mashujaa wa Poland.
Rais Kaczynski alikuwa miongoni mwa maafisa wa kisiasa wa na kijeshi zaidi ya tisini wa Poland waliouwawa wakati ndege yao ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Smolensk nchini Urusi.
Rais Dimitri Medvedev wa Urusi anatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.
Viongozi wengine wengi duniani wamefutilia mbali mipango yao ya kuhudhuria mazishi hayo kutokana na kukwama kwa usafiri wa anga uliosababishwa na majivu ya volcano yanayotimka kutoka Iceland.
0 comments:
Post a Comment