WATOTO WAPONGEZA BUNGE KWA KUPITISHA SHERIA INAYOWALINDA!!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la watoto akionyesha zawadi ya thamani aliyopewa na watoto kwa ajili ya serikali kama shukurani zao kwa serikali na Bunge kutokana na kupitisha muswaada wa sheria ya watoto
mkoani Dodoma leo ambapo zaidi ya watoto elfu mbili wa mkoa huo wamewakilisha watoto wenzao katika tamasha kubwa nchini Tanzania la kupongeza Bunge kwa kupitisha sheria ya kumlinda mtoto
wa Tanzania, Sheria hiyo imepitishwa mwaka jana 2009 na imeanza rasmi kutumika April 1 mwaka huu.. Katika maandamano yaliyopokelewa na Waziri mkuu Mizengo Pinda kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma . Picha zote na Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO.
Waziri wa Jinsia Wanawake na Watoto Mama Margareth Sitta akiangalia vitabu na vitu mbalimbali ambavyo watoto hao walionyesha leo.
Wtoto kutoka shule mbalimbali mkoani dodoma wakishangilia wakati wa tamasha lao leo mjini Dodoma.
Watoto wakiandamana kuingia kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaosema Mtoto ni Uhai wa Familia.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment