Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la umoja wa mataifa UN nchini Kongo wakiwa wamepandisha Bendera za Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kivu.
Wapiganaji wamewaua wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema, waasi wenye silaha nzito wameshambulia mji wa Mbandaka na kuuteka uwanja wa ndege na kuua askari wa kutunza amani wa Ghana na mfanyakazi mwengine wa umoja huo.
Idadi kubwa ya raia pia waliuawa katika shambulio hilo na mpaka sasa haijulikani iwapo majeshi ya kutunza amani ya Umoja wa Mataifa na majeshi ya Kongo yamefanikiwa kuudhibiti upya uwanja huo.
Makundi mawili ya kikabila yanayopingana yanagombea haki ya kuvua samaki eneo hilo.
Mapigano eneo hilo ni tofauti kabisa na ghasia baina ya makundi yenye silaha mashariki mwa Kongo, eneo lililosababisha kuwepo na jeshi kubwa kuliko lote la kutunza amani. http://www.bbcswahili.com/

0 comments:
Post a Comment