Ukonga Bingwa bonanza la Pasaka Ukonga.

Kundi la Bendi ya Mashujaa ambalo limekuwa likitoa burudani kali katika Bonanza hilo linalofanyika kila jumapili katika viwanja vya Magereza Ukonga.
Timu ya Maveterani ya Ukonga ya jijini Dar es Salaam, jana imefanikiwa kuwa Bingwa wa Bonanza la Pasaka la kila mwaka baada ya kuifunga timu ya Veterani ya Arusha( Arusha All Stars) kwa jumla ya bao 2-0.
Bonanza hilo lilishirikisha timu kutoka Zanzibar, Iringa, Arusha,Tanga, na Dar es Salaa, lengo ikiwa ni kuwakutanisha baadhi ya wachezaji wa zamani na kujenga AFYA Mshindi wa kwanza alizawadiwa mipira miwili wakati wa pili yeye alipata mpira mmoja,
Burudani kabambe kutoka katika bendi ya Mashujaa Musica ilikuwa ni moja kati ya Shamrashamra zilizopatikana, ambapo lumba liliporomoshwa chini ya mwanamuziki nyota Elyston Angai, Jado Fidifoce, Ngosha Masanja, Pasia Budansi, Ibrahim Milinda Nyesi, German Kissa, wapiga gitaa Baba Isaya, Amosi Mkono wa Nabii, wacheza shoo Sharony Mapozi, Pendo Bonzo, Flora Bambucha, Mariam Leila Pee,

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment