Mashabiki wenye kushangaa ndiyo hivyo, wenye kucheza nao haya hii ilikuwa ni burudani kabambe kutoka kwa kundi maarufu nchini la African Stars Band wakati lilipofanya onyesho la kukata na shoka kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinondoni usiku wa kuamkia leo wakati wa mkesha wa sikukuu ya pasaka, ambapo mashabiki lukuki walijimwaga ukumbini hapo ili kushuhudia burudani hiyo
Vimwana wa African Stars Bend wakifanya mambo makubwa kama unavyowaona hapa katika picha mdau wa FULLSHANGWE.
Hapa wameambiwa tu mikono juu, lakini hawajaamrishwa kufanya hivyo ni burudani inawasukuma jamani raha siyo mchezo.
Mnenguaji wa African Stars Queen Suzzy ambaye anasadikiwa kuwa ndiye hupandwa na mzuka wa kucheza mara nyingi wakati akiwa jukwaani lakini hata wewe mdau ukimuona )Live) anacheza utakubali mwenyewe.
Dada huyu kwake chupa ya bia haikuwa na usumbufu wowote wa kumfanya asitibwilike na wana wa kutwanga na kupepeta kama unavyomuona.
Mwanamuziki kiongozi wa bend hiyo Lwiza Mbutu akionyesha uwezo wake jukwaani katikati nia Msafiri Diof rapa na Janet Isinika mwimbaji.
0 comments:
Post a Comment