Vyombo vya Habari kupigwa msasa!


Benjamin SaweMaelezoDododma.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mheshimiwa George Mkuchika amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu ,Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshakutana na vyombo vya habari ikiwa ni hatua ya kuvipatia taarifa mbalimbali

Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika taarifa hizo ni pamoja na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura najinsi ya maandalizi yaucgaguzi yanavyokwenda

Alisema tume hiyo pia imepanga kukutana tena na wanahabari kwa mashauriano na kupeana taarifa za maandalizi ya uchaguzi na sheria mpya ya uchaguzi ina kusema kuwavyombo vya habari vinanafasi kubwa ya kuelimisha jamii.

Waziri Mkuchika alisema Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza majukumu yake iliyopewa kisheria katika nyakati tofauti hukutana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya Habari ili kutoa taarifa muhimu zinazohusu mchakato wa uchaguzi.

Pia alisema hadi sasa kuna vituo 58 vya redio na 28 vya televisheni ambapo kati ya hivyo vipo vinavhyomilikiwa na Serikali,watu binafsi,vyama vya siasa,dini na taasisi mbalimbali.
Wakati huo Waziri Mkuchika amewataka wale wote wanaochafuliwa na vyombo vya Habari na hasa magazeti kupeleka lalamiko lake kwake ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Awali Mbunge wa Sumbawanga mjini Mheshimiwa Paul kimiti alitaka kujua ni kwa kiasi gani vyombo vya Habari vimeandaliwa kimafunzo hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi ambapo huwakunatokea vitendo vya chokochoko.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment