Torres kutocheza msimu mzima!!


Mshambuliaji wa Liverpool Fernando Torres hatacheza mechi zilizosalia za kumalizia msimu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Torres alifanyiwa upasuaji siku ya Jumapili nchini Hispania, amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti kwa wiki kadha.

Msemaji wa klabu ya Liverpool amesema: "Imeamuliwa afanyiwe upasuaji katika goti lake la mguu wa kulia na baadae itabidi afuate taratibu za kawaida za kipindi cha wiki sita kuhakikisha anapona vizuri."

Maendeleo yake yatafuatiliwa na meneja wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque, ambapo katika mchezo wa wa kwanza wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini watakumbana na Switzerland tarehe 16 mwezi wa Juni.

Del Bosque anatakiwa kutoa orodha yake ya mwisho kwa Fifa ya majina ya wachezaji 23 watakaoiwakilisha Hispania katika Kombe la Dunia tarehe 1 Juni.

Torres, aliyejiunga na Liverpool akitokea Atletico Madrid mwaka 2007, pia atakosa kucheza mechi za hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Ulaya.

Hadi sasa kwa msimu huu peke yake amekwishafunga mabao 22 katika mashindano yote licha ya kusumbuliwa mara kwa mara na maumivu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment