MISS KURASINI KUZINDUA VODACOM MISS TANZANIA 2010!!

Mratibu wa shindano la Miss Kurasini Bw. Yason Mashaka amesema Shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2010 unaanza rasmi kwa kufunguliwa katika kituo cha Kurasini MISS KURASINI 2010 katika kanda ya Dar es salaam.
Amesema kituo hiki ndiyo kitakuwa cha kwanza kuanza mchakato wa kumvua taji Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald kwa kufanya shindano lake mei 14/ 2010 kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Alli karibu na uwanja wa kimataifa wa Maonyesho ya biashara (sabasaba) Mwalimu J.K. Nyerere.
Amesema mazoezi ya warembo watakaoshiriki kwenye shindano la Miss Kurasini yanaanza kesho aprili 20 /2010 kwenye ukumbi huo wa Equator Grill ambapo yatakuwa yakifanyika kila siku kuanzia saa kumi jioni
Orodha kamili ya warembo watakaoanza mazoezi na mwalimu wao yatatangazwa hivi punde baada ya mazoezi kuanza rasmi.
Taji la Miss Kurasini kwa sasa linashikiliwa na mrembo Shan Antony ambaye pia ni Miss Temeke namba tatu hivyo mrembo huyo alikuwa ni mmoja wa washiriki walioshiriki katika shindano kuu la Vodacom Miss Tanzania 2009

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment