Moja ya picha ikionyesha mlipuko wa Volcano barani Ulaya iliyosababisha jivu kutanda angani na kuleta kikwazo kwa safari za ndege.
Mawiziri wa uchukuzi barani Ulaya wanatarajiwa kufanya mkutano wa dharura kupitia video kujadili mbinu za kurejesha usafari wa ndege barani humo baada ya vikwazo kufuatia jivu la volkano kutanda angani.
Jivu hilo limetokea nchini Iceland. Katika kipindi cha siku nne safari za ndege elfu sitini na tatu zimesimamishwa.
Mamilioni ya wasafiri wamekwama katika viwanja vya ndege kote duniani. Mashirika ya ndege pamoja na wasimamizi wa viwanja vya ndege wamehoji vikwazo hivyo ambavyo vimesababisha hasara inayokisiwa kufikia dola milioni mia mbili kila siku.
Safari za ndege katika anga za mataifa mengi ya bara Ulaya Kaskazini baado zimepigwa marufuku na hadi sasa haijulikani ni lini safari hizo zitaanza tena.
0 comments:
Post a Comment