SIMBA ILIPOISASABUA YANGA GOLI 4-3 NA YANGA WAKAGEUKA WANA KARATEE!!

Nahodha wa Simba Nicodemus Nyagawa (kushoto ) na mlinzi wa timu hiyoJuma Jabu wakishangilia huku wakiwa wambeba Kombe la Ubingwa wa LigiKuu ya Bara mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaamjana.Katika mchezo huo Simba iliicharaza Yanga mabao 4-3. (Picha naMohamed Mambo)
Mbali na ushindi huo Simba ilikuwa inakabidhiwa kombe lake mara baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom msimu huu bila kufungwa hata mchezo mmoja ambapo imeshinda michezo 19 imedroo miwili na bado ina mchezo mmoja mkononi wa kukamilisha ratiba dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu Mkoani Morogoro.
Katika mchezo wa jana wachezaji watatu walipewa kadi nyekundu ambao ni Wisdom Ndlovu na Amir Maftaha wa Yanga baada ya kucheza mchezo mbaya dhidi ya wachezaji wa Simba Salm Kanoni na Juma Kaseja wakati Hilary Echesa wa Simba alipewa kadi nyekundu baada ya kuvua jezi alipokuwa akishangilia goli la nne alilofunga dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji machachari wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi" akishangiliapamoja na wachezaji wenzake goli lake la piloi alilofunga Yanga katikamchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Dar es Salaam jana Mshambuliaji machachari wa Simba Uhuru Seleman akishangilia pamoja nawachezaji wenzake goli la mapema aliloifunga Yanga katika mchezo waLigi Kuu ya Vodacom Dar es Salaam jana Mshambuliaji wa Yanga Jerson Tegete akishangila mara baada ya kufungabao dhidi ya Simba muda mfupi baada ya kuchukua nafasi ya BonifacAmbani.Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 4-3 huku mawiliyakifungwa na Mussa Hassan Mgosi.

Baadhi ya wapenzi wa Yanga wakiwa kimya baada ya matokeo ya kufungwamabao 4--3 na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyikakwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana

Baadhi ya wapenzi wa Simba wakishangilia mara baada ya mpira kwishaambapo timu yao illibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika mchezo wa LigiKuu ya Vodacom uliofanyika Dar es Salaam jana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment